Je, ammonium nitrate ni nini?
Mlipuko mkubwa uliolikumba eneo la bandari ya mji mkuu wa Lebanon, Beirut,
umeishtua dunia nzima, na hadi sasa watu zaidi ya mia moja wamefariki dunia
na wengine elfu nne kujeruhiwa. Imeripotiwa kuwa chanzo cha mlipuko huo ni
tani 2,750 za ammonium nitrate zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala moja
kwa miaka sita bila ya kuzingatia hatua muhimu za kiusalama.