KUJIFUKIZA kwa mvuke wenye mchanganyiko wa mitishamba tofauti kumekuwa gumzo hususani baada ya Rais John Magufuli kushauri wananchi kutumia njia mbalimbali ikiwamo tiba asilia ikiwamo kujifukiza kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).
Wakati wadau wa tiba asilia wakipokea ushauri huo kwa mikono miwili, suala la kujifukiza limetengeneza mjadala mkubwa ulioambatana na jamii kuelekezana mitishamba ya kuchanganya kwa ajili ya kujifukiza.
Maelekezo hayo yamenogeshwa na video mbalimbali za ndani na nje ya nchi zikionesha watu wanaojifukiza baada ya kuchemsha mchanganyiko wa vitu majani na mizizi mbalimbali ikiwamo tangawizi, limao na majani ya miembe.
Miongoni mwa wadau walioeleza kufurahishwa na ushauri wa Rais Magufuli ni Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (Tramepro) cha jijini Dar es Salaam, ambalo limesema ni jukumu la wataalamu na wadau kuja pamoja katika kuilinda na kuihudumia jamii isitumie holela tiba hiyo isije kupata athari nyingine mwilini.
Katibu Mkuu Tramepro, Boneventura Mwalongo alipongeza hatua ya Rais Magufuli kutaka Wizara ya Afya isaidie katika utekelezaji wa tiba hiyo kwa kuelimisha wananchi. Mwanachama Umoja wa Waganga Tanzania ( Uwawata T ) aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kahama, Babu Haji alisema tiba hiyo maarufu kama ‘nyungu’ imeonekana kuvutia watu huku wengine wakifahamu majina na matumizi ya mitishamba ya makabila mbalimbali kwa Akizungumzia kasi ya watu kuelekezana dawa za kujifukiza, Katibu Mkuu wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania (Chawatiata), Mittam Magombeka alisema uwapo wa dawa unategemea na maeneo.
“Ni kweli Kashwagala inapatikana sana Bukoba kutokana na ardhi yao. Lakini kuna mitishamba mingine inaweza kufanya kazi kama hiyo… watu wasije wakahangaika kuifuata dawa mbali maana kila eneo lina miti yake tofauti ambayo pia ni dawa,” alisema na kutaja mchanganyiko wa majani ya mwembe, mdimu, mchaichai kuwa unasaidia.
Wataalamu hao wa tiba asilia walisema kujifukiza si tiba ngeni, bali imekuwapo muda mrefu ambayo mtu yeyote anaweza kujitengenezea hivyo wakahadharisha jamii isije kurubuniwa na watu wachache matapeli wakajitokeza na kudai wanatoa huduma hiyo kwa kutoza fedha. Waganga wa tiba asili na wauzaji wa dawa za asili mkoani Shinyanga, miongoni mwa waliozungumza na gazeti hili na kusema ushauri wa Rais Magufuli na ulivyopokelewa, umedhihirisha jamii ya Watanzania ina uelewa wa tiba hizo.
Mganga wa tiba asilia, Ismail Yusuph alishuhudia wanavyotumia kujivukiza kwa wateja wao wenye matatizo mbalimbali ya kiafya akisisitiza jamii isichukulie utani ni tiba sahihi. Habari hii imeandikwa na Stella Nyemenohi, Dar na Kareny Masasy, Shinyanga.
KUJIFUKIZA kwa mvuke wenye mchanganyiko wa mitishamba tofauti kumekuwa gumzo hususani baada ya Rais John Magufuli kushauri wananchi kutumia njia mbalimbali ikiwamo tiba asilia ikiwamo kujifukiza kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).
Wakati wadau wa tiba asilia wakipokea ushauri huo kwa mikono miwili, suala la kujifukiza limetengeneza mjadala mkubwa ulioambatana na jamii kuelekezana mitishamba ya kuchanganya kwa ajili ya kujifukiza.
Maelekezo hayo yamenogeshwa na video mbalimbali za ndani na nje ya nchi zikionesha watu wanaojifukiza baada ya kuchemsha mchanganyiko wa vitu majani na mizizi mbalimbali ikiwamo tangawizi, limao na majani ya miembe.
Miongoni mwa wadau walioeleza kufurahishwa na ushauri wa Rais Magufuli ni Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (Tramepro) cha jijini Dar es Salaam, ambalo limesema ni jukumu la wataalamu na wadau kuja pamoja katika kuilinda na kuihudumia jamii isitumie holela tiba hiyo isije kupata athari nyingine mwilini.
Katibu Mkuu Tramepro, Boneventura Mwalongo alipongeza hatua ya Rais Magufuli kutaka Wizara ya Afya isaidie katika utekelezaji wa tiba hiyo kwa kuelimisha wananchi. Mwanachama Umoja wa Waganga Tanzania ( Uwawata T ) aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kahama, Babu Haji alisema tiba hiyo maarufu kama ‘nyungu’ imeonekana kuvutia watu huku wengine wakifahamu majina na matumizi ya mitishamba ya makabila mbalimbali kwa Akizungumzia kasi ya watu kuelekezana dawa za kujifukiza, Katibu Mkuu wa Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania (Chawatiata), Mittam Magombeka alisema uwapo wa dawa unategemea na maeneo.
“Ni kweli Kashwagala inapatikana sana Bukoba kutokana na ardhi yao. Lakini kuna mitishamba mingine inaweza kufanya kazi kama hiyo… watu wasije wakahangaika kuifuata dawa mbali maana kila eneo lina miti yake tofauti ambayo pia ni dawa,” alisema na kutaja mchanganyiko wa majani ya mwembe, mdimu, mchaichai kuwa unasaidia.
Wataalamu hao wa tiba asilia walisema kujifukiza si tiba ngeni, bali imekuwapo muda mrefu ambayo mtu yeyote anaweza kujitengenezea hivyo wakahadharisha jamii isije kurubuniwa na watu wachache matapeli wakajitokeza na kudai wanatoa huduma hiyo kwa kutoza fedha. Waganga wa tiba asili na wauzaji wa dawa za asili mkoani Shinyanga, miongoni mwa waliozungumza na gazeti hili na kusema ushauri wa Rais Magufuli na ulivyopokelewa, umedhihirisha jamii ya Watanzania ina uelewa wa tiba hizo.
Mganga wa tiba asilia, Ismail Yusuph alishuhudia wanavyotumia kujivukiza kwa wateja wao wenye matatizo mbalimbali ya kiafya akisisitiza jamii isichukulie utani ni tiba sahihi.